Quinta-feira, 22 de Dezembro de 2011

Jinsi ya Kuzungumza na Mpenzi Wako Aliyekasirika Part I

angry-lovers
Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni cha hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha.

Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya.
Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana.
Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika.

MPUNGUZE MHEMKO

Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano.
Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi.

Soma Jinsi ya Kuzungumza na Mpenzi Wako Aliyekasirika Part II

0 comments:

Enviar um comentário